Usiku wa hamasa 2017 ulifanyika tarehe 1-1-2017 ndani ya ukumbi wa
TUMANYENE SOCIAL HALL uliopo nzovwe, Kuanzia muda wa saa 12 jioni hadi saa 6
usiku.
Mada kuu ya usiku wa hamasa ilikuwa ni UMUHIMU WA KUSIMAMIA KILE UNACHO
KIAMINI NA NIDHAMU YA FEDHA somo hili
lilifundishwa na Mwl Aliko Mwalulili, huku somo la pili lilikuwa ni KUFAHAMU
MAANA YA NDOTO NA VITU MUHIMU KWENYE KUTIMIZA NDOTO somo hili lilifundishwa na
Mc Lawrance Mwantimwa (kutoka . Usiku huu
ulisindikizwa na kauli mbiu isemayo RUKA NA NDOTO YAKO,,,,
Hizi ni baadhi ya picha zikionyesha matukio ya usiku huu wa aina yake;
USIKU WA HAMASA hii ni semina ya ujasiliamali inayo fanyika
kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha watu mbalimbali hususani vijana katika
kutimiza ndoto za maisha yao. Semina hii haijali dini, kabila, jinsia wa itikadi
ya aina yoyote ni kwaajili ya mtu yeyote mwenye kiu na nia ya kujifunza ili
aweze fanikiwa katika maisha yake. DHUMUNI kubwa ikiwa ni kugusa sehemu
zifuatazo-
-kujenga uthubutu
wa vijana katika kutumia fursa kutafuta maisha
-kujijenga
kiuchumi/ biashara
-kujenga
mtandao. Katika kutimiza haya huwa
tunakuwa na mada maalumu ya kuzungumzia na muhamasishaji (muwezeshaji) ambae
huzungumza juu ya mada husika.
Mpaka sasa tumeisha fanya misimu mi nne
ya usiku wa hamasa kwa miaka minne tofauti tokea mwaka 2014, 2015, 2016, na
2017 na kwakila mwaka tumekuwa tukipiga hatua moja kwenda nyingine katika
kufanikisha dhumuni letu la semina hii. Na katika kila mwaka huwa na kauli mbiu
inayosindikiza mafunzo hayo kwa mwaka mzima. Kamavile Una ndoto,Una malengo
JISIKILIZE (2015). Fukuzia ndoto yako (2016),
Ruka na ndoto yako (2017).
NB; mpaka sasa usiku wa hamasa huudhuliwa
na watu wasio pungua 300 wa rika zote vijana na watu wazima.
USIKU WA HAMASA huandaliwa na kampuni
yetu ya EGY BUSINESS SOLUTION na mara kadhaa tumekuwa tukishirikiana na baadhi
ya wadau kama vile TUMANYENE SOCIAL HALL,
FAIDA ZIPATIKANAZO NA USIKU WA HAMASA
kupitia usiku huu wa hamasa kumeonekana kuwa na fursa mbalimbali ambazo watu
huweza kutumia kufafanikisha shughuli zao nazo ni kama:
Watu kutangaza shughuli au biashara zao,
watu kupata hamasa katika kufukuzia ndoto na malengo yao, Watu kuweza kujenga
mtandao kwasababu huwakutanisha watu toka maeneo mbalimbali na nyazfa tofauti,
Lakini pia hutoa fursa ya kufanya biashara pindi semina inapoendelea kufanyika.
Usiku wa hamasa hufanyika jijini Mbeya,
kila mwaka mwanzo au mwisho wa mwaka yaani tarehe 31/12/ au tar 1/01/ kuanzia mda wa saa 12 jioni hadi saa 6 usiku.
Mkurugenzi wa EGY BUSINESS SOLUTION akizungumza na watu ndani ya ukumbi
0 comments:
Post a Comment