.

.

MUNA TOYS & STATIONERY

MUNA TOYS & STATIONERY

Monday, December 8, 2014

NJIA NZURI YA KUWAADHIBU WANAOKUCHUKIA BILA SABABU NI MAFANIKIO ENDELEVU.

MANENO HAYA AMEYAONGEA KIJANA MTANZANIA MWENYE MAFANIKIO ALIYEPITIA CHANGAMOTO NYINGI KATIKA MAISHA NA NDIYE MWALIMU WETU WA KAMPUNI YETU YA EGY BUSINESS SOLUTION,

anza kujifunza polepole uatmuelewa sana
Nasema; njia nzuri ya kuwaadhibu wanaokuchukia si kugombana nao Mtandaoni au kuwanunia au kukunjiana nao ngumi, la hasha, huo ni mtindo wa kizamani sana kumwadhibu mtu anayekuchukia bila sababu, njia ya kisasa ni ipi? KUFANIKIWA SANA NA KUENDELEA KUFANIKIWA KWA MUDA MREFU.


Kwa kipindi kirefu sana niligombana na watu walionichukia bila sababu, tena wengi ni wale ambao hata wakiulizwa "hivi ni kwanini unamchukia Shigongo?" Huwa hawana jibu zaidi ya kusema " hata mimi sijui....ila nalichukia tu" kuna watu huwa wanadhani mimi siumii, naumia sana kwa bunadamu mwingine, haters wamewahi kumitesa sana, baadhi yenu mnajua.
Siku moja nilisoma kwenye kitabu kimoja cheusi kiitwacho Biblia, juu ya mtu aitwaye Yesu, ambaye siku zote nimedai ni rolemodel wangu (ingawa sina uhakika kama naweza kumfia mtu mwingine kama alivyofanya yeye) na kugundua kuwa pamoja na kuwa mtu mwema kwa wayahudi, walimchukia, kumtafutia ubaya na mwisho wakamuua!
Pamoja na yoye hayo hakuwachukia watu hawa, wala kigombana na. Kwake nzima nzuri ya kuwaonyesha alikuwa sahihi haikuwa kubishana wa kupigana nao, bali ilikuwa ni KUFUFUKA KUTOKA KATIKA WAFU, FULL STOP. Alipolifanya hilo, haters wake wote walibaki kimya mpaka leo hii hawana tena cha kusema.
Ndugu yangu unayesoma hapa,


Hata kama wewe ni mwema vipi, siku zote watakuwepo tu watu wanaokuchukia ambao wangetamani hata kuona umekufa! HUU NI UKWELI, YESU ALIKUWA MWEMA LAKINI WALIMUUA IWEJE WEWE? NI UJINGA KUISHI KATIKA MAISHA HAYA UKISEMA " MIMI MGU MWEMA HAKUNA ANAYEWEZA KUNIDHURU"


Hivyo basi Usibisha na haters wala wasikupotezee muda kuwafikiria saaaana, mwisho watakunyong'onyeza na kukuvuta hadi walipo wao ili mlingane na akosekane wa kumsema mwingine, KATAA, WEKEZA NGUVU ZAKO KWENYE NDOTO NA MALENGO YAKO ILI UENDELEEE KUFANIKIWA KWA HIYO NDIO ADHABU NZURI KWA HATERS, ambao wengi husumbuliwa na wivu.


Nayasema haya sababu nina furaha mno kwa mafanikio aliyoyapata Mtanzania Idriss usiku wa jana, ni heshima kubwa kwa taifa letu. Kama unavyojua tena Simba akiwa watu wengi hujipaka damu yake ili waoonekana mashujaa, na mimi ni mmoja wao, nimefurahishwa sana na ushindi wake na ingawa sikumpigia kampeni hapa facebook, sio vibaya kumshangilia kwa ushindi wake ambao mwisho wa siku ni wa kila Mtanzania.

Onyo langu tu kwake ni kwamba, awe makini sana na watu watakaomzunguka kuanzia sasa, awe na uwezo wa kuchuja nani rafiki na nani mpambe! Najua anayo mipango aliyokuwa nayo kabla ya ushindi pengine aliwahi kusema " siku nikipata fedha nita..." Ni vizuri kuyatazama hayo kabla kukurupukia mambo mengine, najua waalimu watakuwa wengi, malengo yakiwa kutumbua.

Namhakikishia, wapo watakaojitolea kumbebea mkoba, kumsifia, kumfungulia mlango wa gari, kumletea wasichana wazuri na kadhalika, anachotakiwa kufanya ni kutulia, fedha na mafanikio ndivyo yalivyo, asibabaike bali ajiamini na kuangalia ndoto zake na kutumia fedha hizi kuzitimiza.
Mafaniko aliyoyapata ni adhabu tosha kwa haters wake, lakini lazima aelewe kuwa adhabu nzuri kwa haters sio tu mafanikio bali Mafanikio Endelevu. Haters ni kama Fungas wakioewa nafasi huchipuka tena.
Yeye sio wa kwanza kushinda fedha hizi, wapo walioshinda kabla yake, wapo wapi? Wanafanya nini? Au wameharibu na kuwapa nafasi haters ya kuendelea kuwaumiza mioyo? Ajifunze kutoka kwa hao na asirudie makosa yao, akumbuke milioni 500 si pesa nyingi tena siku hizi kama iliyokuwa miaka michache iliyopita, akiendeleza starehe na sifa za hapa mjini muda si mrefu akaunti itasoma 000000! Hapo ndipo ataelew kumbe hata waliokuwa wamemzunguka pia walikuwa haters. Itakuwa " yuko wapi ndugu yenu......sisi tulikuwa tunamwangalia tu....bado anaishi kwa mama yake...."
Akumbuke adhabu nzuri kwa haters ni mafanikio makubwa na endelevu.
AMEN.

0 comments:

Post a Comment

 

Bongo Blogs - Blog ya Taifa

COPYRIGHT © Egy business solution DESIGN BY NANG JET 0764504595,0672804085