Baada ya MC ELIUD SAMWEL kusaini mkataba na kujiunga na kampuni
ya EGY BUSINESS SOLUTION siku kadhaa zilizo pita , Sasa ameamua kuja na
programu ya mazoezi ya mwili iendayo kwa jina la MC ELUD TROTAR ambayo
ilizundiliwa rasmi siku ya tarehe 12 -8-2017 ambayo ilikuwa nimaadhimisho ya
siku ya vijana duniani, Programu hiyo itahusisha mazoezi ya mwili kama vile
mbio za kawaida, mazoezi ya viungo na matembezi ya kawaida yote hii ni kwaajili
ya kuuweka mwili salama. Mazoezi hayo yatakuwa yakifanyika kila siku ya
jumamosi kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa mbili ambapo mbio za
kawaida zitakuwa zikianzia eneo la njia panda Halengo au JKT CARWASH kuelekea
uwanja wa mpira wa HALENGO uliopo karibu na kanisa la ROMAN KATOLIKI
shughuli zote zitakuwa ziki malizikia mahali hapo.
MC
ELIUD SAMWEL alielezea
kuhusu programu hiyo yakuwa itakuwa niya mda mrefu na lengo kubwa ni kuwafanya
vijana wa Mbeya kuwa na mazoea ya kufanya mazoezi ya miili yao mara kwa mara ili
kujijenga kiafya. Lakini pia kuwaleta vijana wa Mbeya pamoja ili kufanya mambo
mbalimbali yatakayo leta matokeo chanya kwenye jamii inayo tuzunguka. Nakusema
kuwa anamipango mingi sana kupitia programu hii ambayo itafanyika siku zijazo
pasipo kuizungumzia kiundani mipango hiyo.
Mwisho
aliwashukuru sana watu wote walio muunga mkono katika siku hiyo ya kwanza kwa
kujitokeza kufanya mazoezi hayo na kuanza rasmi kwa kampeni hiyo ya MC ELIUD
TROTAR pia aliwashukuru uongozi wa kampuni ya EGY
BUSINESS SOLUTION kwa kusimamia na kufanikisha shughuli hiyo. Zaidi
alizidi kuwahimiza vijana kujitoa na kuunga mkono programu hiyo kwasababu ina
manufaa kwa kila mmoja atakae shiriki katika kuujenga mwili ili hali kila mmoja wetu anafahamu umuhimu wa
mazoezi katika miili yetu. Kwa maelezo
zaidi kuhusu programu hiyo na ushiriki wake wasiliana nao kupitia namba 0689458877 au 0767187092 na
kuona updates za matukio hayo tembelea kurasa za facebook @MC ELIUD SAMWEL na
instgram @MC_ELIUDSAMWEL_EVENTS na kurasa zote za EGY BUSINESS SOLUTION
0 comments:
Post a Comment