Inawezekana msomaji wetu umekuwa ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakiumiza sana akili kwa kujiuliza maswali mengi juu ya namna gani unaweza kupata wazo zuri ya biashara AU umekua ni mtu unaetamani sana kufanya bishara lakini umekosa kujua ni biashara gani unayo weza kuifanya, Basi leo hii tumekuandalia makala hii kwa ufupi ikieleza juu ya namna unavyoweza kupata wazo la biashara katika nafasi uliyopo, mazingira na vitendea kazi ulivyo navyo:
Njia ya kwanza: NI kutumia fursa (changamoto) zinazo kuzunguka katika jamii. Bila shaka katika kila mazingira tunayo ishi kuna changamoto mbalimbali ambazo zinaikumba jamii zetu basi changamoto izo ni fursa au nafasi nzuri sana ambazo zinaweza kugeuzwa na kuwa biashara unayoweza kuifanya na kukuingizia kipato na pia kutatua tatizo ambalo jamii yako ilikuwa inasumbuliwa nalo. Mfano unaweza kuangalia ni kitu gani katika mazingira unayoishi au mazingira jirani kinahitajika sana na watu lakini upatikanaji wake umekuwa wa shida sana inaweza kuwa bidhaa au huduma , ukiisha fahamu ilo ni muhimu sasa kuchuka maamuzi ya kutafuta namna ya kutatua tatizo ilo kwa kuleta bidhaa au huduma hiyo na kuigeuza kuwa biashara yako.
Njia ya pili: NI kutumia ujuzi au kipaji ulicho nacho. Kama ni mtu ambae una ujuzi wa vitu mbalimbali Mfano ujuzi wa kushona, kusuka, ufundi wa vitu mbalimbali basi hiyo ni njia bora zaidi ya kugeuza kuwa bishara yako ambayo unaweza kufanya kwa ubora zaidi na ukawa unakulipa. Lakini pia kipaji au talanta uliyo nayo ndio njia kubwa zaidi ya kuitumia kama biashara kama unaweza kuimba,kuchora,kucheza,kuigiza kuandika stori n.k. Muhimu ni namna unavyoweza kukaa chini na kufikilia juu ya namna unavyvo weza kugeuza kipaji chako na kuwa biashara. Bahati nzuri ujuzi sio kitu ambacho lazima uwe umezaliwa nacho kama kipaji ila ni kitu ambacho unaweza ukajifunza kwa watu mbalimbali hivyo basi usiache kujifunza vitu kwasababu katika ujuzi ndiko unakoweza kupata wazo zuri na bora zaidi ya kupata biashara unayoweza kuifanya.
Njia ya tatu: NI kucopy biashara ambayo inafanyika na watu wengine. Nikweli kuwa duniani hakuna kitu kipya kila jambo tunaloliona tayri limewahi kufanywa kabla nawatu wengine, Hivyo basi si kitu kibaya kama utaweza kucopy biashara ya mtu mwingine ila tu kitu cha msingi ni juu ya namna ambvyo utaweza kujitofautisha na watu wengine kwa kuongeza ubunifu na kufanya biashara hiyo kwa namna ya tofauti na mazingira tofauti. Mfano unaweza kucopy biashara kutoka nchi nyingine na kuifanya mpya katika mazingira yako n.k.
Njia ya nne: NI kutumia teknolojia kuanzisha biashara. Katika ulimwengu huu tulio nao wa kidigitali, teknolojia imekuwa ndio kitu muhimu zaidi na inayokuwa kwa kasi Hivyo basi watu wamekuwa wakiraisisha maisha kwa kutumia teknolojia huku wakiitumia kama biashara. Nawe pia unayo nafasi ya kutumia teknolojia kuwa biashara kwako, Mfano tumeona watu wakitengeneza mkaa kwa kutumia makaratasi hapo kilicho tumika ni ujuzi na teknolojia basi nawewe anza kujiuliza kama ni mtu unae weza au mtaalamu wa kitu fulani kinachohusu teknolojia, Anza sasa kuitumia teknolojia hiyo kama biashara. Mfano angalia mfumo wa maisha ya sasa ,vitu vinavyotumika na namna ambavyo teknolojia inaweza kuboresha au kurahisisha alafu ifanye kama biashara.
Njia ya tano: NI kutumia njia zote za kiutafiti kupata wazo la bishara Mfano kupitia maonyesho ya bishara,magazeti, mitandao na taasisi zinazo husu biashara.
Nafikili kupitia njia hizo tano kuna njia moja inaweza kuwa msaada mkubwa kwako na ikakupatia majibu ya maswali yako ambayo ulikuwa ukijiuliza kwa mda mrefu, sisi tunakutakia kila lakheri katika utekelezaji wa hayo yote uliyo yapata.
Usiache kutembelea blog yetu kwa mafunzo mbalimbali kila siku na kushare kwa watu wengine ili ujumbe huu uweze kufika mbali zaidi na kuwasaidia watu wengine. pia unaweza ku comment ilituweze kupata maoni yako. Ahsante sana
0 comments:
Post a Comment