Siku chche zilizo pita vijana wa mbeya walipata fursa ya kushiriki katika semina na mdahalo unao husu katiba , Semina hiyo iliandaliwa na shirika lisilo la kiselikali la TANZANIA YOUTH VISION ASSOCIATION (TYVA) KUTOKA JIJINI Dar es salaam kushirikiana na IRI. Katika semina hiyo vijana walijifunza mambo mengi yanayo husu katiba kamavile maaana ya katiba historia ya katiba ya Tanzania tokea ilipoanzishwa hadi kufikia hatua ya kutaka kutengeneza katiba mpya maarufu kama katiba pendekezwa na mahali ilipofikia mpaka sasa.
Semina hiyo ilifanyika siku tatu ambapo siku ya kwanza ilikuwa ikiwahusu zaidi waandishi wa habariwa jiji la mbeya kupitia vyombo mbalimbali vya habari kamavile radio, magazeti, blog, n.k Katika siku hii wandishi wa habari walifundishwa juu ya namna waandishi wa habari walivyo na nafasi kubwa kaktika kuelimisha na kutoa taarifa sahihi juu ya katiba kupitia vyombo vyao vya habari hivyo basi walipewa elimu kiundani zaidi kuhusu katiba.
siku ya pili na ya tatu iliwahusisha vijana wa mbeya mjini na mbeya vijijini huku itifaki ikizingtiwa ilikuweka usawa wa jinsia, dini, vyama vya siasa n.k. Katika semina hiyo ilihusisha na mdahalo ambao uliwapa nafasi vijana kushriki kiundani zaidi kwa kuuliza maswali ili kujua uelewa wa vijana hao juu ya katiba yao hasa katiba pendekezwa, Hivyo basi vijana walipewa nafasi ya kuuliza maswali ili kuwasaidia kuwapa uelewa zaidi. Lakini pia muwezeshaji alitoa elimu juu ya haki za binadamu hususani watu wenye uhitaji maalumu kama vijana, wazee , wanawake, watoto na walemavu na namna katiba ilivyowaelezea watu hao na mapungufu yaliyoko katika katiba ya Tanzania juu ya watu hao
Kila kijana alionyesha kufurahia semina hiyo na kuomba taasisi zingine kuendelea na programu hizo za kutoa elimu juu ya katiba na haki za binadamu pasipo kusibili kipindi fulani chenye vuguvugu za kisiasa kama vile kipindi cha uchaguzi. Shukrani ziwaendee sana TYVA kwa semina hii kwa vijana na waandishi wa habari ndani ya mkoa wa Mbeya.
Usiache kutembelea blog yetu kwa mafunzo na matukio mbalimbali kila siku na kushare kwa watu wengine ili ujumbe huu uweze kufika mbali zaidi na kuwasaidia watu wengine,,. Pia unaweza ku comment ilituweze kupata maoni yako. Ahsante sana
MUNA TOYS & STATIONERY

Browse » Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment