Kuchoma meli moto (BURN THE BOAT) ni falsafa ambayo ilikuwa ikitumiwa na
jeshi la wagiriki ANCIENT GREEK WARRIOS
miaka ya nyuma falsafa hii iliwajenga
wanajeshi hawa kufanya bidii zote na hatimaye kushinda kila vita waliyokuwa
wanapigana miaka hiyo
Wanajeshi hawa walipokuwa wanaenda kupigana vita na nchi nyingine kutokana na zamani ilikuwa sio rahisi kwa wao kutumia ndege kwao njia iliyokuwa rahisi ni kutumia meli kwa kubebea wanajeshi pamoja na silaha zao,
Walipofanikiwa kufika ng’ambo ya maadui zao yaani ng’ambo ya
nchi nyingine, njia pekee kamanda wao wa
jeshi alichowaamuru ni kuichoma
meli yao ambayo iliwasaidia kufika ng’ambo na wao kubaki na silaha pekee, na kuanza mapambano na maadui zao,
wao tukio hili kwao la kuchoma meli (BURN THE BOAT) lilikuwa
na maana kubwa kwao kwani liliwajaza nguvu ya kuendelea kupambana kwani kurudi
nyuma au kufanya utegezi wa namna yoyote
ile kwao kusingewasaidia kitu kwani usafiri ulio wawezesha wao kufika ng’ambo
hiyo ulikuwa umeisha teketea kwa moto
Hivyo njia pekee iliyowabakia ni kupambana au kufa yaani
(COMPETE OR DIE) kwani ilikuwa hamna njia nyingine ya kusalimika kwao kwani meli
ilikuwa haipo,hii iliwajenga katika vitu kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwa
1.
HAKUNA KUKATA TAMAA (kwani hata ukikata tamaa
usafiri wa kukurudisha nyumbani haupo)
2.
HAKUNA KURUDI NYUMA (meli haipo)
3.
HAKUNA KUJITETEA WALA KUJISALIMISHA KWA ADUI
Wanajeshi
waliposhuhudia meli zao zikichomwa moto akili zao zilichojaa ni kupambana mpaka
washinde , kwani kulikuwa hamna njia mbadala
KATIKA MAISHA YETU
Tumekuwa tukikutana na vikwazo vingi sana katika maisha yetu
hivyo kutufanya kuto kusonga mbele aidha ya kuogopa kuchekwa na marafiki, ndugu
na kukatishwa nao tamaa , na wengi wameshindwa kuendelea mbele katika maisha
kwa sababu ya kuogopa kufanya maamuzi ya vitu wanavyo viamini katika ndoto zao,
Wengi wa marafiki zetu wamekuwa wakitusimulia mipango na
ndoto walizonazo ila imekuwa shida kwao
kuanzisha na kuanza kuzitenda. Sasa njia sahihi kwako ni KUCHOMA MELI MOTO kwa
jambo unalotaka kulianzisha yaani amua kulifanya kwani kurudi au kutazama nyuma
hakuta kusaidia,
Vijana wengi tumekuwa na ndoto za kuanzisha vitu mbalimbali
ila tumekuwa tukikumbwa na ugonjwa mkubwa ambao unaitwa FEAR(HOFU) ambayo njia
sahihi ukitaka kufanikiwa katika ndoto zako ni wewe kuamua KUCHOMA MELI YAKO YA
HOFU MOTO na kuiamini ndoto na malengo na amua leo kuanza na kuanzisha hilo
jambo unaloliamini,
Unania ya kuingia katika ujasiriamali, biashara ya namna
yoyote ni kipindi chako cha sasa kuamua KUCHOMA MELI MOTO nakuingia rasmi huku
ukiamini ndoto zako na kamwe usitazame watu ambao wameshindwa au wanao
kukatisha tamaa kikubwa ni kuto kataa na tumia falsafa ya WAGIRIKI
kwao meli kuwepo pembeni ilikuwa ikiwatia uvivu, kwahiyo kwao njia bora ni kuzichoma meli moto
0 comments:
Post a Comment