Kila mwaka mkoani Mbeya maadhimisho ya NANENANE huwa yanafanyika katika viwanja vya MWAKANGALE vilivyopo jijini Mbeya ambapo watu mbalimbali huwa wanajitokeza katika kutazama na kusherekea maadhimisho ya sikukuu ya Wakulima
Ambayo kwa kanda ya kusini hufanyikia katika jiji la Mbeya.Sasa kuna watu ambao wanatarajikia katika maonesho haya na wengine wanaingia na kutoka bila ya kupata chochote,mara zote huwa tunafundisha hivi MAFANIKIO NI NAMNA YA WEWE UNAVYOONA! UKIPAMBANA KUONA TOFAUTI NA MTAZAMO CHANYA UTAFANIKIWA TUU
KIJANA FANYA HAYA KWA AJILI YA MAONESHO YA NANENANE
1.TENGENEZA BUSINESS CARD/VIPEPERUSHI
Ikiwa una kitu chochote ambacho unashughulika nacho katika jamii ikiwa ni pamoja na biasharazako ulizo nazo, au we ni mwanasanaa ,mkulima, au kuna kitu ambacho unakifanya,
Tengeneza vipeperushi ambavyo vitakuelezea kitu unacho kifanya kavigawe kwa mashirika na watu ambao ni muhimu kwako, Fanya hivyo kijana itumie hii fursawatu wafahamu unachokifanya
2.KAKUSANYE TAARIFA ZA WATU WENGINE
Jijengee tabia ya kujifunza kwa wengine sasa Nanenane hii fanya jambo hili nenda kakusanye taarifa wengine wanafanyeje na wametumia mbinu gani walipofikia
3.KAJENGE MTANDAO WA KUFAHAMIANA NA WENGI
Hii ni fursa kwako kijana kutengeneza mtandao wa watu wenye Malengo na ndoto kama zako, jenga mtandao wa kutosha sana , MATIJIRI WANAPAMBANA KUTENGENEZA MTANDAO MARA ZOTE, kwahiyo usikubali kupita Nanenane bila ya kutengeneza Mtandao
4.KATHUBUTUU/ KAJARIBU
Amua hii Nanenane iwe ya kwako kuthubutu na kujaribu sana sana ukiisha kujifunza na kuona UENDE KUTHUBUTUU, kataa huu mwaka usiwe wa wewe kushangaa tuu NENDA KATHUBUTUU
YOTE HAYA NI MATUKIO NA UJUMBE KUTOKA
cc EGY BUSINESS SOLUTION
PHONE+255764761900
MUNA TOYS & STATIONERY

Browse » Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment