1. KUWA NA NDOTO
Ndoto ni jambo kubwa sana na la thamani kama tuu utalipa umuhimu yake
unayoitarajia katika kufikia mafanikio yako, ili usiwezwe kukatishwa tamaa cha
kwanza tafuta ndoto unayoitaka maishani mwako , na ilinde kisawasawa, hii
itakuongoza na kukujulisha kuwa unakwenda wapi? Na pia unataka kufika wapi?
2. FIKIRI KWA
KIWANGO KIKUBWA
Hakuna uvivu mbaya kama kuwa na uvivu wa kufikiria, tena hususani kufikiria
kila mara kwa mtazamo hasi na tena kwa kiwango kidogo, mara zote unapokuwa na
ndoto jaribu sana kufikiria kwa kiwango kikubwa, hii njia itakuongoza wewe
kufanya vitu kwa kiwango cha juu zaidi na kuyafikia yale uyatakayo kwa urahisi.
ACHA KUFIKIRIA KIKAWAIDA KAWAIDA
3. ANZA KIDOGO
Anza mahali ulipo na kwa kiwango ulichonacho, hata kama unaona mafanikio
makubwa mbele yako ambayo unaweza uone kuwa ni ngumu kuyafikia, Iamini sehemu
unayoelekea ,usihofu kwenda kidogo kidogo, wachina wana kauli yao huwa wanasema
HATUOGOPI KWENDA POLEPOLE TUNACHOOGOPA
KUSIMAMA MAHALI TULIPO
4. JIAMINI MWENYEWE
Makosa makubwa unayoyaendelea kuyafanya ni pale ambapo HAUJIAMINI
MWENYEWE na kutokuziamini ndoto na
malengo yako, Acha kusubiria watu wanje wakuamini ndiyo uanze . huwa waswahili
tunasema KAMA USIPOJIAMINI MWENYEWE, NANI AKUAMINI?
5. JIANDAE KUPINGWA
Haijalishi unaanzisha jambo la namna gani katika maisha haijalishi ni
jambo lenye manufaa yako mwenyewe au kwa lengo la kubadiri dunia, yaani watu wa
kukupinga watatokea tuu, hii ni ujumbe ninaoweza kukuachia WEE JISIKILIZEE NA
JIELEWE MWENYEWE ACHA WAJE WAPINGAJI
6. JIFUNZE KUCHUKUA
TAHADHARI
Unapoanzisha jambo au umefanikiwa kutengeneza jambo lolote katika maisha
jaribu kuwa na tahadhari,Hii itakuongeza kufanya jambo kwa umakini na mafanikio
zaidi
0 comments:
Post a Comment