Tumekuwa tukitafuta namna mbalimbali ambazo tunaweza kuyafanya maisha yakawa mazuri zaidi kuliko tuliyonayo kwa sasa, sisi kama EGY BUSINESS SOLUTION tunakuletea hizi sababu kwa uchache tuu namna ya wewe kuyafurahia maisha yako, kama ifuatavyo
WAPE WATU ZAIDI YA WANAVYOTEGEMEA
Mara nyingi watu wanategemea kuwa uwezo wako utakomea kwenye eneo flani, huku wakijijengea uhakika wa asilimia zote kuwa siajabu utaishia pale, lakini jambo kubwa sana ambalo ukitaka kuyafurahia haya maisha ni wewe kufanya jambo zaidi hata ya wengine wanavyotegemea , BINADAMU WANAHAMU KUBWA SANA KUWA UISHIE PALE WANAPOPAONA WAO. Usitishike hata kama wao wanasema mara kwa mara JIAMINI WEWE NA FANYA ZAIDI YA WANAVYOTEGEMEA
KAMA UNAMPENDA MTU BASI MAANISHA
namna yoyote ya kufikia furaha ya ndani mwako ni kujenga upendo kwa binadamu wanaokuzunguka na ikitokea unampenda mtu yeyoto hakikisha UNA MAANISHA, hata ukipata nafasi ya kumwambia unampenda hakikisha inatoka ndani kabisa
ACHA KUYAAMINI YOTE AMBAYO UNAYASIKIA
Mara nyingi katika ongea yetu tumekuwa tukisisitiza sana namna tunavyokutana na sauti nyingi sana humu duniani, hivyo na mpaka mwisho wa dunia tutasikia mengi, ila chunga sana kuyaamini yote unayoyasikia, kila sauti inaweza kukuambia la kwake na zitakuja za kukutia moyo, kukatisha tamaa, USIAMINI KILA SAUTI UNAZOZISIKIA
USICHEKE AU USIMCHEKE MTU YEYOTE
KUHUSIANA NA NDOTO ZAKE
Kila binadamu anacho kitu ambacho anakiona
ndani mwake na kiu ya mafanikio anayotaka kuifikia usijaribu kuanza kuicheka na
kuidharau, haujui nguvu ambayo ameiweka kuifanikisha ndoto yake.kuna msemo huwa
unasemwa USICHEKE JAMBO USILOLIJUA MWISHO WAKEIKIWA UMEJUA KUWA UMEKOSEA, CHUKUA HATUA YA KUJIREKEBISHA
Hakuna binadamu ambaye hajawahi kufanya makosa kikubwa tulichotofautiana ni viwango na aina ya makosa tuliyoyafanya , sasa makosa kwako yaweke kama somo na amini kuwa upo dunia darasa hivyo kukosea ni jambo a kawaida sana. Kikubwa sana kwako ni hili hapa unapobaini kuwa umekosea basi ichukue hatua ya haraka KUREBISHA UTAFANIKIWA
MUDA MWINGINE JIPE MUDA WAKUKAA MWENYEWE, UJUE KITU CHA KUIPA DUNIA
kukaa muda mwingine peke yako kunakupa
furaha sana, kwani unakuwa na muda mzuri wa kuipa dunia na kujua ufanye nini
kwa ajili ya watu wengine na wewe pia , hatimaye kuelekea mafanikio yale
uyatakayo katika uhai wako
AHSANTENI
KARIBUNI KUFANYA KAZI PAMOJA NA SISI KATIKA MAMBO MBALIMBALI
0 comments:
Post a Comment