.

.

MUNA TOYS & STATIONERY

MUNA TOYS & STATIONERY

Sunday, January 4, 2015

SAFARI YANGU KWA MWAKA 2014. NA TUNAVYOWEZA KUWA PAMOJA 2015

ELLY L BONKE, hivi ndivyo safari yangu ya mwaka 2014 nilivyoimaliza na kuanza kuiwaza safari yangu ya mwaka 2015 nitaifanikishaje hata ikiwezekana ikawe bora zaidi ya mwaka 2014,

Kiujumla safari ilikuwa nzuri kwa upande wangu licha ya kuwa na changamoto nyingi nyingi sana , ambazo zilikuwa zikijitokeza katika mwaka 2015. lakini huwa naamini DUNIA INASUBIRIA NIFANYE KITU NISIPOFANYA KWAHIYO LAZIMA NIFANYE
Ikiwa hata bado kufikisha miaka 25, ya kukaa kwangu hapa duniani huwa napenda kufanya kazi pamoja na watu kwa kushirikiana pindi tuu, pale watakapohitaji kufanya kazi na mimi au ikiwa utahitaji kufanya kazi na taasisi ambazo nashughulika nazo

1.Niko tayari kufanya kazi na vikundi vyovyote vya vijana, iwapo vina lengo la kuleta mabadiliko chanya katika jamii, naweza nisiwe mshiriki wa moja kwa moja ila nikawa mshauri wao

2.Nafanya shughuli na mashirika mbalimbali na pia nipo tayari kufanya na shirika lolote ikiwa tutakuwa na makubaliano maalumu

3.Niko tayari kufundisha kikundi chochote cha jamii au vijana, kuhusiana na changamoto mbalimbali ambazo tunazipitia duniani

4.Niko tayari kushiriki tukio lolote ambalo limeandaliwa lenye lengo la kuleta mabadiliko chanya kwa dunia, kama mijadala, semina

ILA KATIKA HIVI HAPA CHINI HUWEZI UKANIKUTA NIKISHIRIKI

1.Naheshimu kila mmoja na kazi yake ila huwa sishiriki tukio lolote ambalo litachanganyika na UNYWAJI POMBE, NA STAREHE ZOZOTE ZISIZO NA KUJENGA

2.Naheshimu wasanii zaidi ya sana HUWA SISHIRIKI AINA YOYOTE YA DISKO, ikiwa hujaniona ujue ni aina na mfumo wa maisha nilojiwekea

katika mwaka 2014 nimejaribu kuwa sehemu tuu ya watu ambao tulijaribu kuleta vitu ambavyo vilikuwa ndani yetu na hizi hapa ndiyo kazi ambazo unaweza ukanialika tukafanya pamoja nami au kupitia taasisi ninazofanya kazi nazo
1.EGY  BUSINESS SOLUTION  hii ni kampuni ambayo nasimama kama DIRECTOR  ambayo mpaka sasa ina mwaka na nusu toka rasmi kuianzisha na hatimaye kuwa na usajiri kwa mwaka huu,unaweza kututafuta katika UMC'S
                          UANDAAJI WA MATUKIO( EVENT MANAGEMENT)
                          UHAMASISHAJI & NA UTOAJI ELIMU (MOTIVATIONAL SPEAKER)
                          JISIKILIZEE.BLOGSPOT.COM
                          UKODISHAJI VITI VYA PLASTIC
2.MLIMANI YOUTH GROUP, nashukuru Mungu nikiwa bado kama mwanzilishi wa kikundi hiki ambacho kina shughulika na matukio mbalimbali ya kijamii na yale yanayoweza kutuletea kipatoo tumeweza kufanya mengi mwaka huu, pia unaweza kufanya kazi pamoja nasi

3.YWCA MBEYA na WAJIBIKA PROJECT MBEYA, nikiwa mwanachama na mmoja kati ya waandaaji wa project mbalimbali kwa mwaka 2014 kupitia WAJIBIKA, ambazo kiukweli zimekuwa mabadiliko sana kwa jamii ya mbeya, katika maeneo mbalimbali niliofanya kazi na project hii, tunawakaribisha kufanya kazi pamoja nasi zaidi na zaidi

4.MBEYA YOUTH, hii ni taasisi ambayo inamuhusisha kijana yoyote ambaye anatamani na kuwa na nia ya kujiletea maendeleo yeye mwenyewe na jamii inayomzunguka, nikisimama kama MRATIBU wa tukio la mwaka 2014, na pia tunawakaribisha kwa tukio la mwaka 2015, ambalo litakuwa ni zaidi ya mwaka 2015

ni mengi sana nashukuru kwa taasisi ya SAUTI YA MAMA AFRIKA FOUNDATION(MBEYA). CWS YOUTH( EAST AFRICA) kwa kushirikiana nao vyema. FOUNDATION CIVIL SOCIETY( TANZANIA) bila kusahau UWEZO chini ya TWAWEZA, tuishie hapo

NIZISHUKURU REDIO KWA KUNIPA SUPPORT YA MIMI KUSIKIKA AU TAASISI NILIYOPO KAMA VILE : SWEET FM, HIGHLANDS FM, BARAKA FM, USHINDI FM, ROCK FM

PICHA ZA MATUKIO NILIYOSHIRIKI KWA MWAKA 2014, NYINGINE ZIKIWA ZA KUSTAAJABU KWANGU NA KUONA KAMA MUUJIZA

    Mwaka 2014 nimefanikiwa kupanda mlima kilimanjaro mpaka kilele cha mwisho kabisa UHURU PEAK
  Nikiwa mratibu wa event ya vijana kwa Mbeya, iliyokwenda kwa jina MBEYA YOUTH EVENT
Mwaka jana ziarani ya kutafiti juu ya tukio la vijana linalokuja mwaka 2015 kwaajili ya vijanaUSIKOSEE
     KIWIRAA

                       Wilaya ya Rungwe nikiwa nafanya event ya mazingira, tukuyu
                 ziara ya LAKE NGOSI pamoja na MBEYA HOME TOURISM

                                            Nikiwa na mkuu wa wilaya ya Rungwe
                                                       tukio la kupanda miti mlima loleza
                          Nikila chakula na watoto walioondokewa na wazazi wao
                                 Nikiwa na wanaclub wa mazingira shule ya mapinduzi
                            Nikiwa na wanaclub ya mazingira shule ya sekondari nzondahaki
                               Ndani ya hospitali ya Rufaaa tulipowatembelea wagonjwa
                                   Ndani ya MBEYA HIGHLANDS FM
                                       Pamoja na katibu tawala wa WILAYA YA MBEYA
                   Dar es salaam , nikiwa pamoja na FOUNDATION CIVIL FOR SOCIETY
                                        Mwaka mmoja wa kikundi cha MLIMANI
                                  Nikifanya usafi katika hospitali ya wazazi META
                                                                 BARAKA FM
              Tukipoenda kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu katika shule ya kilimahewa
                                                 KAULI MBIU YA MWAKA 2015
KWA NAMNA YOYOTE UKIHITAJI KUFANYA KAZI NA MIMI AU TAASISI NILIZOPO UNAKARIBISHWA SANA SANA,
ZAIDI YA YOTE NASHUKURUNI KWA SUPPORT YENU KWA MWAKA 2014,
TUSICHUKIANE, TUOMBEANE, DUNIA INASUBIRIA MAWAZO YETU KUIBADILISHA
    KWA UCHACHE HAYO NDIYO , MATUKIO KWA UCHACHE NIMEONA NIYAWEKE
FB: ELLY L. BONKE             EMAIL:ellybonke7@gmail.com       0764761900

0 comments:

Post a Comment

 

Bongo Blogs - Blog ya Taifa

COPYRIGHT © Egy business solution DESIGN BY NANG JET 0764504595,0672804085