.

.

MUNA TOYS & STATIONERY

MUNA TOYS & STATIONERY

Thursday, September 28, 2017

JINSI YA KUPANGA MIPANGO AU MALENGO YANAYOTEKELEZEKA,,

0 comments
Kuna watu hujituma sana katika kutafuta maisha lakini katika juhudi zao hawaonekani wafanya kitu cha maana au wakifanikiwa yote hii husababishwa na kuto kuwa na mipango thabiti na mizuri inayo tekelezeka , Hivyo wamejikuta wakitumia nguvu nyingi kutafuta lakini wamekuwa hawajui wanatafuta nini. Hali hii hufananishwa na mtu anae enda safarini bila kujua ni mahali gani anapokwenda hivyo safari yake huwa haina mwisho na hujikuta kila njia aionayo mbele yake kuifuata pasi kujua ni wapi inampeleka. Ndio maana leo tumekuletea somo hili juu ya namna ya kupanga mipango inayotekelezeka ili katika kila juhudi zako zionyeshe ni nini unacho kipagania.



Hatua ya kwanza: Tengeneza picha kubwa juu ya kitu unachotaka kufanya kwenye maisha yako. Hapa namaanisha kuwa katika akili yako lazima uwe na ufahamu juu ya kitu unacho taka kukifanya au unachotaka kukiona kinafanyika maishani mwako,, picha ambayo itasimama kama ndio ndoto ya maisha yako. picha hii itabeba kusudi la maisha yako, katika vitu vingi tunavyoona duniani vikifanyika vilianza katika hatua hii. Muhimu ni kuwa picha hii lazima iwe kubwa kwaakili za kawaida.

Hatua ya pili: Ni kubadili picha kuwa lengo kuu au kubwa zaidi la maisha yako (destination). Katika hatua hii unaanza kubadilisha ndoto au maono yako kuwa mpango utakao tekelezeka na kuifanya kuwa uhalisia. hatua hii haitofautini sana na hatua ya kwanza ila hapa ni muhimu zaidi kwasababu ni mahali ambapo mawazo hugeuzwa kuwa uhalisia na kuonekana kwa kila mtu , katika hatua hii ndio hufanya ndoto (mawazo) ya watu wengi kuishi miaka mingi kwasababu hata wanapokufa kuna watu huwa wanakuja kuendeleza iwapo mtu huyo aliishia sehemu fulani.

Hatua ya tatu: Ni kuligawa lengo kuu  katika vipengele, ukisha fahamu juu ya lengo kuu la maisha yako katika hatua ya pili ni muhimu sasa kuligawa lengo hilo katika vipengele vidogovidogo ambavyo vitalenga kufikia lengo kuu. Mfano lengo unaweza ukagawa katika miaka yaani baada ya miaka au mda fulani niwe nimetimiza kufanya jambo fulani ambalo litakuwa linaelekea kutimza lengo kuu.  lazima ufahamu namna ya kuvipanga na namna ya kuvifanya ili kutimiza malengo yako. Panga mipango ya miaka mitano, kila mwaka, kila baada ya miezi sita hata mwezi mmoja kama inawezekana na hakikisha kila mpango unahusiana na mpango uliopita.

Baada ya kupanga malengo yako zingatia yafuatayo:

-Hakikisha malengo hayo umeyaandika tena sehemu unayoweza kuiona kula siku au unayoweza kuisoma kila siku unapolala na unapo amka, hii itakupa hamasa zaidi ya kuyatimiza.

-Weka malengo yenye uharisia na yanayoweza kutimilika. Lazima uweke malengo ambayo yako chini ya uwezo  wako na yanaweza kutimilizika. pasi nakuwa hakuna kisicho wezekana lakini ni  muhimu pia kuangalia aina ya lengo kama linawezekana katika level uliyopo.

-Weka vipaumbele katika malengo yako. Katika mipango uliyo weka nilazima ufahamu kuwa kunampango lazima umfuate mwenzake yaani moja liwe na kupaumbele zaidi kuzidi lingine. kwahiyo yapange katika mfumo huo.

-Hakikisha unaweka orodha ya ratiba ya mambo unayotakiwa kufanya kila siku ili kutimiza lengo lako la maisha.

-Weka muda maalumu wakutimiza lengo yako, kwa maaana kwamba uweze kufahamu kama umefanikisha au uemefeli kutimiza lengo lako.

-Usikate tamaa katika kuipigania mipango yako, changamoto ni nyingi sana utazo kutana nazo unapokuwa ukipambana kuhkikisha malengo yako yanatimia hivyo unaweza kushindwa mara kadhaa au mambo kuonekana magumu, Fahamu tu yakuwa hiyo hli ni yakawaida muhimu tu ni kuto kata tamaa na kuamini kuwa iko siku malengo yako yatatimia.



Usiache kutembelea blog yetu kwa mafunzo mbalimbali kila siku na kushare kwa watu wengine ili ujumbe huu uweze kufika mbali zaidi na kuwasaidia watu wengine. pia unaweza ku comment ilituweze kupata maoni yako. Ahsante sana
SOMA ZAIDI ...

Wednesday, September 27, 2017

FAHAMU NAMNA YA KUPATA WAZO ZURI LA BIASHARA

0 comments

Inawezekana msomaji wetu umekuwa ni miongoni mwa watu ambao  wamekuwa wakiumiza sana akili kwa kujiuliza maswali mengi juu ya namna gani unaweza kupata wazo zuri ya biashara AU umekua ni mtu unaetamani sana kufanya bishara lakini umekosa kujua  ni biashara gani unayo weza kuifanya,  Basi leo hii tumekuandalia makala hii kwa ufupi ikieleza juu ya namna unavyoweza kupata wazo la biashara katika nafasi uliyopo, mazingira na vitendea kazi ulivyo navyo:



Njia ya kwanza: NI kutumia fursa (changamoto) zinazo kuzunguka katika jamii. Bila shaka katika kila mazingira tunayo ishi kuna changamoto mbalimbali ambazo zinaikumba jamii zetu basi changamoto izo ni fursa au nafasi nzuri sana ambazo zinaweza kugeuzwa na kuwa biashara unayoweza kuifanya na kukuingizia kipato na pia kutatua tatizo ambalo jamii yako ilikuwa inasumbuliwa nalo. Mfano unaweza kuangalia ni kitu gani katika mazingira unayoishi au mazingira jirani kinahitajika sana na watu lakini upatikanaji wake umekuwa wa shida sana inaweza kuwa bidhaa au huduma , ukiisha fahamu ilo ni muhimu sasa kuchuka maamuzi ya kutafuta namna ya kutatua tatizo ilo kwa kuleta bidhaa au huduma hiyo na kuigeuza kuwa biashara yako.

Njia ya pili: NI kutumia ujuzi au kipaji ulicho nacho.   Kama ni mtu ambae una ujuzi wa vitu mbalimbali Mfano ujuzi wa kushona, kusuka, ufundi wa vitu mbalimbali basi hiyo ni njia bora zaidi ya kugeuza kuwa bishara yako ambayo unaweza kufanya kwa ubora zaidi na ukawa unakulipa. Lakini pia kipaji au talanta uliyo nayo ndio njia kubwa zaidi ya kuitumia kama biashara kama unaweza kuimba,kuchora,kucheza,kuigiza kuandika stori n.k. Muhimu ni namna unavyoweza kukaa chini na kufikilia juu ya namna unavyvo weza kugeuza kipaji chako na kuwa biashara. Bahati nzuri ujuzi sio kitu ambacho lazima uwe umezaliwa nacho kama kipaji ila ni kitu ambacho unaweza ukajifunza kwa watu mbalimbali hivyo basi usiache kujifunza vitu kwasababu katika ujuzi ndiko unakoweza kupata wazo zuri na bora zaidi ya kupata biashara unayoweza kuifanya.
Njia ya tatu: NI kucopy biashara ambayo inafanyika na watu wengine.  Nikweli kuwa duniani hakuna kitu kipya kila jambo tunaloliona tayri limewahi kufanywa kabla nawatu wengine, Hivyo basi si kitu kibaya kama utaweza kucopy biashara ya mtu mwingine ila tu kitu cha msingi ni juu ya namna ambvyo utaweza kujitofautisha na watu wengine kwa kuongeza ubunifu na kufanya biashara hiyo kwa namna ya tofauti na mazingira tofauti. Mfano unaweza kucopy biashara kutoka nchi nyingine na kuifanya mpya katika mazingira yako n.k.

Njia ya nne: NI kutumia teknolojia kuanzisha biashara. Katika ulimwengu huu tulio nao wa kidigitali, teknolojia imekuwa ndio kitu muhimu zaidi na inayokuwa kwa kasi Hivyo basi watu wamekuwa wakiraisisha maisha kwa kutumia teknolojia huku wakiitumia kama biashara. Nawe pia unayo nafasi ya kutumia teknolojia kuwa biashara kwako, Mfano tumeona watu wakitengeneza mkaa kwa kutumia makaratasi hapo kilicho tumika ni ujuzi na teknolojia basi nawewe anza kujiuliza kama ni mtu unae weza au mtaalamu wa kitu fulani kinachohusu teknolojia, Anza sasa kuitumia teknolojia hiyo kama biashara. Mfano angalia mfumo wa maisha ya sasa ,vitu vinavyotumika na namna ambavyo teknolojia inaweza kuboresha au kurahisisha alafu ifanye kama biashara. 

Njia ya tano: NI kutumia njia zote za kiutafiti kupata wazo la bishara Mfano kupitia maonyesho ya bishara,magazeti, mitandao na taasisi zinazo husu biashara.
Nafikili kupitia njia hizo tano kuna njia moja inaweza kuwa msaada mkubwa kwako na ikakupatia majibu ya maswali yako ambayo ulikuwa ukijiuliza kwa mda mrefu, sisi tunakutakia kila lakheri katika utekelezaji wa hayo yote uliyo yapata.

Usiache kutembelea blog yetu kwa mafunzo mbalimbali kila siku na kushare kwa watu wengine ili ujumbe huu uweze kufika mbali zaidi na kuwasaidia watu wengine. pia unaweza ku comment ilituweze kupata maoni yako. Ahsante sana

SOMA ZAIDI ...

TAZAMA "UELEWA WA VIJANA WA MBEYA KUHUSU KATIBA YA NCHI"

0 comments
Siku chche zilizo pita vijana wa mbeya walipata fursa ya kushiriki katika semina na mdahalo unao husu katiba , Semina hiyo iliandaliwa na shirika lisilo la kiselikali la TANZANIA YOUTH VISION ASSOCIATION (TYVA) KUTOKA JIJINI Dar es salaam  kushirikiana na IRI. Katika semina hiyo vijana walijifunza mambo mengi yanayo husu katiba kamavile maaana ya katiba historia ya katiba ya Tanzania tokea ilipoanzishwa hadi kufikia hatua ya kutaka kutengeneza katiba mpya maarufu kama katiba pendekezwa na mahali ilipofikia mpaka sasa.

Semina hiyo ilifanyika siku tatu ambapo siku ya kwanza ilikuwa ikiwahusu zaidi waandishi wa habariwa jiji la mbeya kupitia vyombo mbalimbali vya habari kamavile radio, magazeti, blog, n.k Katika siku hii wandishi wa habari walifundishwa juu ya namna  waandishi wa habari walivyo na nafasi kubwa kaktika kuelimisha na kutoa taarifa sahihi juu ya katiba kupitia vyombo vyao vya habari hivyo basi walipewa elimu kiundani zaidi kuhusu katiba.

siku ya pili na ya tatu iliwahusisha vijana wa mbeya mjini na mbeya vijijini huku itifaki ikizingtiwa ilikuweka usawa wa jinsia, dini, vyama vya siasa n.k. Katika semina hiyo ilihusisha na mdahalo ambao uliwapa nafasi vijana kushriki kiundani zaidi kwa kuuliza maswali ili kujua uelewa wa vijana hao juu ya katiba yao hasa katiba pendekezwa,     Hivyo basi vijana walipewa nafasi ya kuuliza maswali ili kuwasaidia kuwapa uelewa zaidi. Lakini pia muwezeshaji alitoa elimu juu ya haki za binadamu hususani watu wenye uhitaji maalumu kama vijana, wazee , wanawake, watoto na walemavu na namna katiba ilivyowaelezea watu hao na mapungufu yaliyoko  katika katiba ya Tanzania juu ya watu hao

Kila kijana alionyesha kufurahia semina hiyo na kuomba taasisi zingine kuendelea na programu hizo za kutoa elimu juu ya katiba na haki za binadamu pasipo kusibili kipindi fulani chenye vuguvugu za kisiasa kama vile kipindi cha uchaguzi.   Shukrani ziwaendee sana TYVA kwa semina hii kwa vijana na waandishi wa habari ndani ya mkoa wa Mbeya.


Usiache kutembelea blog yetu kwa mafunzo na matukio mbalimbali kila siku na kushare kwa watu wengine ili ujumbe huu uweze kufika mbali zaidi na kuwasaidia watu wengine,,. Pia unaweza ku comment ilituweze kupata maoni yako. Ahsante sana
SOMA ZAIDI ...

Friday, September 22, 2017

USIKU WA HAMASA 2017

0 comments
            
Usiku wa hamasa 2017 ulifanyika tarehe 1-1-2017 ndani ya ukumbi wa TUMANYENE SOCIAL HALL uliopo nzovwe, Kuanzia muda wa saa 12 jioni hadi saa 6 usiku.
Mada kuu ya usiku wa hamasa ilikuwa ni UMUHIMU WA KUSIMAMIA KILE UNACHO KIAMINI NA NIDHAMU YA FEDHA  somo hili lilifundishwa na Mwl Aliko Mwalulili, huku somo la pili lilikuwa ni KUFAHAMU MAANA YA NDOTO NA VITU MUHIMU KWENYE KUTIMIZA NDOTO somo hili lilifundishwa na Mc Lawrance Mwantimwa (kutoka .   Usiku huu ulisindikizwa na kauli mbiu isemayo RUKA NA NDOTO YAKO,,,,
Hizi ni baadhi ya picha zikionyesha matukio ya usiku huu wa aina yake;

USIKU WA HAMASA  hii ni semina ya ujasiliamali inayo fanyika kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha watu mbalimbali hususani vijana katika kutimiza ndoto za maisha yao. Semina hii haijali dini, kabila, jinsia wa itikadi ya aina yoyote ni kwaajili ya mtu yeyote mwenye kiu na nia ya kujifunza ili aweze fanikiwa katika maisha yake. DHUMUNI kubwa ikiwa ni kugusa sehemu zifuatazo-
                             -kujenga uthubutu wa vijana katika kutumia fursa kutafuta maisha
                             -kujijenga kiuchumi/ biashara
                             -kujenga mtandao.     Katika kutimiza haya huwa tunakuwa na mada maalumu ya kuzungumzia na muhamasishaji (muwezeshaji) ambae huzungumza juu ya mada husika.
Mpaka sasa tumeisha fanya misimu mi nne ya usiku wa hamasa kwa miaka minne tofauti tokea mwaka 2014, 2015, 2016, na 2017 na kwakila mwaka tumekuwa tukipiga hatua moja kwenda nyingine katika kufanikisha dhumuni letu la semina hii. Na katika kila mwaka huwa na kauli mbiu inayosindikiza mafunzo hayo kwa mwaka mzima. Kamavile Una ndoto,Una malengo JISIKILIZE (2015). Fukuzia ndoto yako (2016),  Ruka na ndoto yako (2017).
NB; mpaka sasa usiku wa hamasa huudhuliwa na watu wasio pungua 300 wa rika zote vijana na watu wazima.

USIKU WA HAMASA huandaliwa na kampuni yetu ya EGY BUSINESS SOLUTION na mara kadhaa tumekuwa tukishirikiana na baadhi ya wadau kama vile TUMANYENE SOCIAL HALL,
FAIDA ZIPATIKANAZO NA USIKU WA HAMASA kupitia usiku huu wa hamasa kumeonekana kuwa na fursa mbalimbali ambazo watu huweza kutumia kufafanikisha shughuli zao nazo ni kama:
Watu kutangaza shughuli au biashara zao, watu kupata hamasa katika kufukuzia ndoto na malengo yao, Watu kuweza kujenga mtandao kwasababu huwakutanisha watu toka maeneo mbalimbali na nyazfa tofauti, Lakini pia hutoa fursa ya kufanya biashara pindi semina inapoendelea kufanyika.
Usiku wa hamasa hufanyika jijini Mbeya, kila mwaka mwanzo au mwisho wa mwaka yaani tarehe 31/12/ au tar 1/01/  kuanzia mda wa saa 12 jioni hadi saa 6 usiku.
                                                              


Mkurugenzi wa EGY BUSINESS SOLUTION akizungumza na watu ndani ya ukumbi




                                                                                         
SOMA ZAIDI ...

Thursday, August 17, 2017

"MC ELIUD TROTAR" PROGRAMU YA MAZOEZI INAYOKUJA KWA KASI

0 comments

Baada ya MC ELIUD SAMWEL kusaini mkataba na kujiunga na kampuni ya EGY BUSINESS SOLUTION siku kadhaa zilizo pita , Sasa ameamua kuja na programu ya mazoezi ya mwili iendayo kwa jina la MC ELUD TROTAR ambayo ilizundiliwa rasmi siku ya tarehe 12 -8-2017 ambayo ilikuwa nimaadhimisho ya siku ya vijana duniani, Programu hiyo itahusisha mazoezi ya mwili kama vile mbio za kawaida, mazoezi ya viungo na matembezi ya kawaida yote hii ni kwaajili ya kuuweka mwili salama. Mazoezi hayo yatakuwa yakifanyika kila siku ya jumamosi kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa mbili ambapo mbio za kawaida zitakuwa zikianzia eneo la njia panda Halengo au JKT CARWASH kuelekea uwanja wa mpira wa HALENGO uliopo karibu na kanisa la ROMAN KATOLIKI shughuli zote zitakuwa ziki malizikia mahali hapo.

MC ELIUD SAMWEL alielezea kuhusu programu hiyo yakuwa itakuwa niya mda mrefu na lengo kubwa ni kuwafanya vijana wa Mbeya kuwa na mazoea ya kufanya mazoezi ya miili yao mara kwa mara ili kujijenga kiafya. Lakini pia kuwaleta vijana wa Mbeya pamoja ili kufanya mambo mbalimbali yatakayo leta matokeo chanya kwenye jamii inayo tuzunguka. Nakusema kuwa anamipango mingi sana kupitia programu hii ambayo itafanyika siku zijazo pasipo kuizungumzia kiundani mipango hiyo.

Mwisho aliwashukuru sana watu wote walio muunga mkono katika siku hiyo ya kwanza kwa kujitokeza kufanya mazoezi hayo na kuanza rasmi kwa kampeni hiyo ya MC ELIUD TROTAR pia aliwashukuru uongozi wa kampuni ya EGY BUSINESS SOLUTION kwa kusimamia na kufanikisha shughuli hiyo. Zaidi alizidi kuwahimiza vijana kujitoa na kuunga mkono programu hiyo kwasababu ina manufaa kwa kila mmoja atakae shiriki katika kuujenga mwili  ili hali kila mmoja wetu anafahamu umuhimu wa mazoezi katika miili yetu.    Kwa maelezo zaidi kuhusu programu hiyo na ushiriki wake wasiliana nao kupitia namba 0689458877 au 0767187092 na kuona updates za matukio hayo tembelea kurasa za facebook @MC ELIUD SAMWEL na instgram @MC_ELIUDSAMWEL_EVENTS na kurasa zote za   EGY BUSINESS SOLUTION




            Hapa ndio JKT CARWASH mahali ambapo mazoezi huanzia kuelekea viwanja vya Halengo



                                  Viwanja vya Halengo mazoezi yalipo anza.














            Mc Eliud Samwel akitoa maelezo baada ya mazoezi

                      Baada ya mazoezi baadhi ya washiriki wakipata picha ya pamoja.
SOMA ZAIDI ...

Friday, August 11, 2017

JIONEE "MC ELIUD SAMWEL" ALIVYOJIUNGA RASMI EGY BUSINESS SOLUTION

0 comments
Siku ya tarehe 25 mwezi wa 7 mwaka 2017 ni siku ambayo MC ELIUD SAMWEL alikuwa anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa. Katika siku hiyo ni mengi yalifanyika katika warsha ndogo aliyo iandaa na kufanyika katika ukumbi wa TS STUDIO uliopo NZOVWE, MBEYA  mambo hayo yaliacha kumbukumbu kubwa katika maisha yake .

Kubwa katika yote ambalo lilionekana kufuraisha wageni walio alikwa katika warsha hio na MC ELIUD ni pale alipo tangaza rasmi na kuwatumia wageni waalikwa kama mashaidi na kutangaza rasmi yakuwa kuanzia siku hiyo atakuwa akifanya kazi rasmi na kampuni ya EGY BUSINESS SOLUTION kama mshereshaji wa matukio mbalimbali ya ndani ya kampuni na nje ya kampuni kamavile semina,mikutano, na nje ya kampuni ni kama harusi, sendoff, birthday parties, graduations, n.k au shughuli yoyote inayo hitaji mshehereshaji.  Katika kuthibitisha hayo akasaini mkataba mbele ya wageni waalikwa na tukio hilo likisimamiwa na mkurugenzi wa EGY BUSINESS SOLUTION ndugu ELLY BONKE na atakae kuwa meneja wake (MC)  ndugu EMMANUEL MWANSASU .

Mwisho kabisa ni nafasi aliyo tumia MC ELIUD SAMWEL kuwaomba watu wote kumuamini na kumpa nafasi ya kusheheresha shughuli/sherehe zao   na kuwa ahidi kuwa atafanya kazi kwa utofauti na kwa ubora zaidi na kuacha mawasiliano yao.
                                                           
                                            Mawasiliano;  0764761900
                                                                    0767181092







                                              wageni mbalimbali wakishiriki ukataji wa keki

         Mkurugenzi wa EGY BUSINESS SOLUTIONS ( ELLY BONKE)  akitia saini makubaliano


    Team ya EGY kulia ni IMANUEL MWANSASU, ELIUD SAMWEL, ELLY BONKE, SHEDU

          LILIAN BONKE kwa niaba akikabidhi makataba wa kampuni



                     MKURUGENZI WA TS STUDIO AKIWA NA MC ELIUD SAMWEL
SOMA ZAIDI ...

Thursday, October 6, 2016

YOUTH CAMP IN MBEYA,30 SEPTEMBA 2016.....MATUKIO YOTE YAKO HAPA JIONE

0 comments
YOUTH CAMP IN MBEYA 30 SEPTEMBER 2016......ilikuwa siku pekee kwa vijana kukutana na kuzungumza katika masuala mazima ya Ujasiriamali,Uongozi,Kujitambua. na Namna ya kusimamia ndoto za vijana .
Maisha yalikuwa ya kuishi na kuzungumza pamoja hususani kujenga mtandao kwa vijana wa kitanzania , kuwa na uelewa kuhusiana na jamii kwa ujumla. washiriki mbalimbali walishiriki kutoka ndani ya mkoa wa Mbeya na Nje ya Mbeya
Kupitia taasisi ya MBEYA YOUTH INITIATIVE wakiwa waandaji wa CAMP hii ya hamasa yalizungumzwa Mengi ya kumuondoa kijana hatua moja kwenda nyingine
Mawasiliano
Ukihitaji kukutana na taasisi hiii
Facebook....MBEYA YOUTH INITIATIVE
Instagram .....mbeyayouthinitiative
Youtube.......MBEYA YOUTH
Simu.....0764761900 au 0718972260
                      Hapa ni Nje Ndani muda ulipowadia wa mazoezi ya pamoja
                         Chai mapema asubuhi kila mtu na kikombe chake



                                 Mada mbalimbali zikitolewa na vijana wakijadiri

                           Jinsi unavyongeza mtandao ndivyo unavyokaribia utajiri wako
ALPHA AGUSTINO akitoa somo la uonoziwa Familia na Maisha kwa ujumla kwa vijana
                 Maisha ya kuzungumza pamoja na kucheza pamoja ni muhimu kwa vijana

                          Unaweza kusimamia ndoto yako ukiamua kuwa mtu wa tofauti na sasa




SOMA ZAIDI ...
 

Bongo Blogs - Blog ya Taifa

COPYRIGHT © Egy business solution DESIGN BY NANG JET 0764504595,0672804085