.

.

MUNA TOYS & STATIONERY

MUNA TOYS & STATIONERY

Sunday, March 8, 2015

VIJANA KUTOKA YOUNG PEACE PERFORMERS ( YPP) WAKIWA NCHINI TANZANIA, MKOA MBEYA KUELEKEA DARAJA LA MUNGU

Ziara ya vijana wa YOUNG PEACE PEFORMERS kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Srilanka, Palestina, Norway, na Kenya umeweza kuwasili katika jiji la mbeya kupitia usimamizi wa YWCA MBEYA ambao umekuja kwa lengo la kuendeleza kampeni yao kuu ya STOP POVERTY huku ukilenga kukutana na makundi mbalimbali ya vijana kwa ajili ya kujifunza kutoka kwao na pia vijana wa hao kujifunza kwa watanzania

Safari yetu ikaanzia katika ofisi za UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES ambapo wageni wetu wakaweza kukutana na chifu mkuu wa kabila la wasafwa Mwanshinga pamoja na machifu wengine,

KUELEKEA  DARAJA LA MUNGU
Mara baada ya kumaliza kushuhudia ngoma ya kisafwa,Tukaanza  Ziara yetu kutembelea kivutio cha asili cha Daraja la mungu ambapo safari hii ilisimamiwa na    Uyole Cultural Tourism Enterprises kwa usimamizi wa kiongozi wa safari AMOC ASAJILE,  ambao wanapatikana eneo la uyole,
unaweza kuwasiliana nao zaidi kwa ajili ya kushuhudia vivutio zaidi EMAIL; 
Uyolecte@gmail.com

Bila kusahau TEAM TANZANIA ilikuwepo( IMANUEL MWANSASU, JULIUS JAILO, JOSEPH GEORGE, DEBORA NJULUMI, ERIC) katika ziara hii tukiongozwa na blog yako ya  www.jisikilizee.blogspot.com na mpiga picha ELLY BONKE karibu ushuhudie

                                               Tukiondoka eneo walilofikia wageni wa YPP
                                        Tulipotembelea supermarket eneo la mwanjelwa


 


                          Tukiwasili katika ofisi za Uyole Cultural Tourism Enterprises


 Vijana wakicheza ngoma ya asili ya wasafwa
Tukipewa maelekezo kuhusiana na kaburi walilozikwa watu wengi njia ya kwenda Tukuyu, kutokana na ajali ya moto iliyotokana kuanguka kwa roli la mafuta
Daraja kuleeee safari inaendelea

                                                   Julius, Amoc, Imanuel, Eric
                                              Ndani ya daraja la mungu tayari
                                                             Chini ya daraja la mungu

YACOB pamoja na NEEMA ndani ya daraja la mungu kiwira mbeya
 Naona vijana wa YWCA na UYOLE CULTURAL TOURISM wakifurahia jambo
tukiondoka daraja la mungu
Neema akielezea vyakula vya asili vilivyopo

Debora Njulumi project officer wa WAJIBIKA MBEYA akishiriki chakula cha asili cha watu wa mkoa wa mbeya kilichoandaliwa na UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES
PICHA NA MATUKIO: ELLY BONKE
KARIBUNI SANA NA ENDELEA KUTEMBELEA www.jisikilizee.blogspot.com

1 comments:

  1. Tunashukuru sana YWCA na YPP kwa kuweza kutembelea vivutio vya kitalii mkoani mbeya, Karibuni tena Tanzania YPP.

    ReplyDelete

 

Bongo Blogs - Blog ya Taifa

COPYRIGHT © Egy business solution DESIGN BY NANG JET 0764504595,0672804085