TEAM CHALLENGE,
SAFARI YA VIJANA WA KITANZANIA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO.KWA LENGO LA KUPAZA SAUTI ZAO ZISIKIKE
YMCA world Alliance yenye makao mkuu Geneva, Switzerland pamoja na baraza la vijana la YMCA Tanzania lenye makao yake makuu mjini moshi, chini ya uratibu wa kampuni la vijana wa kitanzania TANPICTURES UNIVERSAL waliandaa tukio kubwa kwa vijana nchini Tanzania waliandaa tukio na kushiriki wiki ya vijana iliyopewa jina la Y’s VOICE SUMMIT ndani ya siku saba kuanzia tarehe 02.06.2014 hadi 08.06.2014
Ambayo vijana wa kitanzania waliungana na vijana
zaidi ya milioni 58 toka nchi zinazounda umoja
wa YMCA (world Allience). Jambo muhimu ni kuunga mkono kaulimbiu ya
vijana itakayowezesha mabadiliko sahihi ya uundwaji sera za kimaendeleo kuanzia
ngazi ya nchi hadi dunia.
Hii ni pamoja na vijana watanzania kupata fursa ya kueleza
mawazo, hisia na maoni yao katika mambo makuu yaliyopewa kipaumbele ni pamoja
na SERA UWEZESHWAJI, NAFASI YA KIJANA KATIKA UONGOZI NA MASUALA YAHUSUYO AFYA
na AJIRA hasa suala la ajira binafsi kwa njia ya kipaji
Maadhimisho haya ya siku ya vijana dunia yalihusisha vijana
kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania ikiwa ni pamoja na vijana kutoka MBEYA,
TANGA, MOSHI,DAR ES SALAAM, ARUSHA, DODOMA,MANYARA, ambao kwa pamoja waliweza
kufanikisha wiki ya vijana duniani na
Wadhamini wakuu wa
safari hii ni kampuni bora la utalii ZARA(WWW.ZARATOURS.COM)
lililopo mjini moshi, na AZAM na supermarket ya kisasa ya MARENGA
MADHUMUNI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
1.kuwahamasisha vijana
watanzania na kupandisha bendera yenye ujumbe wa mwaka 2014 kwenye kilele cha mlima
Kilimanjaro kwa ishara na alama ya kusikika
2.kutangaza utalii na utamaduni wetu kwani watu wengi
watashuhudia hili likifanyika kwenye kilele hiki ambacho ni kivutio kwa wengi
‘NASIMAMA KWA AJILI
YA VIJANA NA NINATAKA SAUTI YAO ISIKIKE’
Team challeng vijana wakiwa YMCA TANZANIAvijana walipopata fursa ya kutembelea kampuni bora la utalii ZARA(www.zaratours.com) mjini moshi
TEAM CHALLENG kwa mwaka 2014 walipandia njia ya marangu hapa ndipo safari ilipo anzia wakiwa na kiu ya kufika kilele cha mlima mrefu barani africa
njiani ilikuwa furaha tuu na nyimbo kwa pamoja
vijana TEAM CHALLENG wakiwa HOROMBO mita 3720 kutoka usawa wa bahari
ZEBRA ROCKS ni eneo la kuvutia sana lenye hali ya ubaridi na rahisi kukiona kilele cha mawenzi kwa urahisi
GILMAN'S point eneo la juu kabla ya kufikia uhuru peak
vijana wakifanya maombi ya kumshukuru MUNGU kwa kufika eneo la juu kabisa la mlima kilimanjaro UHURU PEAK
KIFUNIKA eneo linalofanyiwa maombi kwa kiimani na kufanyika matambiko mbalimbali
0 comments:
Post a Comment