UMESHINDWA MARA NGAPI MPAKA HUTAKI
KUENDELEA TENA? Ni
swali kubwa na gumu ambalo kwa siku ya leo tumependa kukuuliza wewe ambaye
unafuatilia blog yetu “JE UMESHINDWA MARA NGAPI MPAKA HUTAKI KUENDELEA TENA?
JE UMESHINDWA
MARA NGAPI?
Na wengi wetu wamekuwa wakishindwa mara moja,
mara mbili au hata mara kumi na kurudi nyuma na kusahau kabisa ndoto zao na
malengo yao ,na hii imechangia sana dunia ya leo kuwa na watu wengi ambao wanafanya vitu ambavyo kiukweli sio msukumo
wao wa moyoni , na kikubwa tena unakuta wameshindwa kwenye hatua ya mwanzo
kabisa katika maisha yaani katika “plan A”.
hebu leo yazingatie haya maneno, unataakiwa kuzingatia sana maneno haya
kama unataka kufanikiwa katika mipango na ndoto zako
Kwahiyo unayosababu
sana kwako kujishangaa jinsi ulivyokata tamaa kwenye hatua ya mwanzo tuu,
wakati hata hatua ya pili ujaijaribu, ndiyo maana tunakuuliza” umeshindwa mara ngapi hata hutaki kuendelea tena?”
Hebu
yatazame maneno kwa uchache ambayo MICHAEL JORDAN mwanamichezo maarufu dunia na
mwanzilishi wa wa staili mbalimbal iza uchezaji wa basketball nchini marekani alivyokuwa akisisitiza suala
la kutokata tamaa
Watu wengi waliofanikiwa katika maisha ni watu
walioshindwa na kushindwa lakini walipambana na ndoto zao hatimaye wakafanikiwa
, ndiyo maana hatutokubaliana sana na sababu zako za kusema huwezi kuendelea
tena mbele, kwani umeshindwa mara nyingi je inatosha kushindwa kwako huko ndiyo
usiendelee tena mbele
Mwisho
tunapenda kukuacha na maneno haya yaende kukujenga na usijipe sababu tena ya
wewe kutokuendelea mbele, maadamu mambo kwako hayajakaa sawa ujue sio mwisho
endelea kupambana mpaka upate. MAFANIKIO MEMA KWAKO KWA KUENDELEA KUSOMA BLOG
YETU
0 comments:
Post a Comment