Watu
wengi waliofanikiwa duniani na ambao hawajafanikiwa dunia huwa tunatofautiana
sana kwa vitu vidogo na hakuna suala la uchawi wala kurogana katika kufikia
mafanikio yaliyo ya ukweli. Namna ambavyo namna yetu ya kuishi ilivyo na
nidhamu basi ndiyo vinatufanya tutaofautiane wengine wawe matajiri na wengine
masikini
Nayasema
haya huku nikihusianisha maisha aliyokuwa na tajiri wa kwanza duniani ndugu
BILL GATES hivi sasa na hapo awali, hii inaonesha ukiamua kucheza mchezo vizuri
wa kutafuta mafanikio ya kweli hapo haina upinzania lazima ufanikiwe tuu,
tunaona kuwa BILL GATES ni mtu aliyeshindwa sana darasani na katika maisha na
siajabu hata kuzadharauliwa, lakini alipoamua kubadirisha maisha yake na
hatimaye akawa namna alivyo sasa
Mtu
mwingine ambaye naye anaonesha namna ambavyo ukiamua kubadirisha mfumo wa
maisha uwezavyo ni ERICK SHIGONGO.
Shigongo ambaye historia yake inaonesha kuwa alipitia vipindi vigumu vy a
kudharauliwa na kusemwa vibaya kutokana na ufukara alio kuwa nao lakini hivi
leo ni miongoni mwa vijana wanaosikilizwa sana Tanzania na tajiri,kikubwa
aliamua kubadilisha historia ya maisha yako, sasa hivi hapa chini ni
VITU
VINNE KWAKO MUHIMU KUFIKIA MAFANIKIO YAKO YA KWELI
PAMBANA
KUBADILI MATOKEO: unapoelekea kufikia mafanikio yako kuna kitu ambacho unakiona
mbele yako ambacho unaamini ukifanikiwa kukibadili basi mafanikio yako
yanatokea sasa ushauri ambao ninaweza kukupatia ni wewe kupambana kuyabadili
matokeo mabaya yanayokuzunguka na kuweka mtazamo mwingine mpya
IJUE
THAMANI YA MUDA WAKO: watu waliofanikiwa na mara nyingi huwa wanajiuliza kipi
cha thamani nianchotumia muda huu , jaribu kuupa muda thamani yake usiuache
upotee bure mbele yako na kuiacha siku ipite bila ya wewe kufanya jambo lenye
maana
WEKA
VIPAUMBELE: duniani na tunavyotembea njiani tunakutana na vitu vingi sana na
siajabu kila kitu tunatamani kuvifanya lakini jambo la muhimu ambalo unapaswa
kulifahamu yote hayo uwezi kufanya kwa wakati mmoja bila ya kuweka vipaumbele
vyako, kwahiyo jaribu kuwa na vipaumbele vyako katika maisha
FANYA
KILA JAMBO KWA UFANISI: onesha ubora wako
katika kila jambo ambalo unalifanya hii itakuwezesha wewe kuwa bora
zaidi na wakipekee na utajikuta unaelekea katika mafanikio yako, haijarishi
hilo jambo ni lako ama la watu Fulani ili mradi tuu umepewa nafasi ya kulifanya
wewe litekeleze kwa bidii yako yote utafikia mafanikio yako
AHSANTE
KWA KUENDELEA KUJIFUNZA PAMOJA NASI, WEWE NI BORA NA UNAUWEZO WA KUBADILISHA
DUNIA
0 comments:
Post a Comment