.

.

MUNA TOYS & STATIONERY

MUNA TOYS & STATIONERY

Friday, October 17, 2014

HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJIAJIRI KAMA KIJANA





 Kijana yoyote ambaye unaisoma makala hii ambaye unataka kujiaajiri kwanza lazima uyazingatie mambo haya , kwanza uelewe ujasiriamali ni kitu cha namna gani na unawezaje kufanikiwa kupitia ujasiriamali.

MJASILIMALI ni mtu Yule ambaye anakuwa na uwezo wa kuyasoma mazingira na kuweza kuyatumia na kuyafanyia biashara, na  ni mwepesi sana kuliko hata wengine,

Na pia ni mtu ambaye anauwezo wa kuthubutu, kubuni, kuanzisha na kuendesha biashara au mradi wa namna yoyote utakao mwingizia kipato chake 

 Tunasaidiana pamoja na wewe kufahamu mbinu mbalimbali ambazo zitakusaidia kujiajiri tuzisome pamoja

1.kijana unatakiwa kufahamu kuwa maisha yako unaetakiwa kuyaongoza na kuyastawisha ni wewe mwenyewe na wala sio mtu mwingine kama Wazazi, marafiki au mamlaka yoyote , hao wengine watakusaidia kuyafikia yale uliyoyapanga kama kijana

2.JIAMINI,  kikubwa kama kijana unatakiwa kujiamini katika yote uyapangayo na katika lolote ulitakalo kulifanya ili mradi tuu litaleta mabadiriko chanya katika maisha yako

3. UWE MTAMBUZI WA FURSA, kijana unapaswa kuwa mtambuzi wa fursa ambazo zinakuzunguka na uwe na uwezo kuzitumia katika kujiajiri kwani dunia imejaa fursa nyingi ambazo kama kijana unaweza kuzitumia na zikakuingizia kipato chako cha kila siku

4. JIFUNZE KUWEKEZA, unaweza ukawa unawekeza katika kipato lakini kikubwa jifunze kuwekeza  katika fani na ujuzi mbalimbali ambazo zitakuwezesha katika kujiajiri , hivyo ujuzi na ufundi mbalimbali utakuwezesha wewe kuyafikia mafanikio yako katika maisha

5. WEKA DIRA NA MALENGO,  hivi vitu vitakusukuma sana katika kuyafikia mafanikio yako katika kujiajiri kwani vitakuongoza pale unapotaka kuelekea na kuwa mbunifu  zaidi katika yale unayotakiwa kuyafikia 

6. USIKATE TAMAA,  unahitaji kuwa na moyo wa kijasiri zaidi kama kweli umedhamilia kuwa mjasiliamali kwani ni hatua ambayo unatakiwa kutokata tamaa kirahisi, maisha yamejaa changamoto nyingi sana katika dunia hauhitaji kukata  tamaa.

7. ANZA MAHALI ULIPO, kijana hebu acha kujichelewesha na kusubirisha ndoto zako  ,jifunze kuanza mahali ulipo, kwani katika maisha kuanza ndiyo  kitu muhimu 

8. ONGEZA UVUMILIVU, mafanikio hayaji siku moja kijana yoyote ambaye unasoma makala yetu hii ujue fika mafanikio hayaji usiku mmoja unatakiwa kuwa mvumilivu, pindi unapotaka kuyafikia mafanikio

AHSANTE TUNAAMINI UMEJIFUNZA KUPITIA MAKALA HII AMBAYO IMELETWA KWAKO NA 

          MOTIVATIONAL SPEAKER KUTOKA EGY BUSINESS SOLUTION

0 comments:

Post a Comment

 

Bongo Blogs - Blog ya Taifa

COPYRIGHT © Egy business solution DESIGN BY NANG JET 0764504595,0672804085