Kitendo cha
kuhairisha jambo na kulipa muda wa siku nyingine au wakati unao uwezo wa
kufanya kwa wakati uliopo, limekuwa tatizo kubwa kwa wengi na limesababisha
kutokuweza kufika ndoto za wengi
hususani vijana wengi huu ugonjwa ndiyo tunaouita PROCASTINATION
Sababu kubwa
zinazofanya wengi wetu kuhailisha mambo na kutokufanya kwa wakati na kujikuta wanangukia
katika ugonjwa huu ni pamoja na
·
UOGA WA KUANZA
Wengi na karibia kila binadamu hapa duniani anayo ndoto ya kufikia mahali
fulani ila kitu kikubwa ambacho kimekuwa kikikwamisha ni UOGA WA KUANZA na
kujikuta kila siku anasogeza jambo husika mbele, na kutokulifanya kwa wakati
sahihi.
·
KUSIKILIZA SANA WENGINE,TOFAUTI YA
UNAVYOJISIKILIZA
Hili pia limekuwa tatizo kubwa kwa wengi na hasa vijana kusikiliza sana
wengine mpaka wakuambie ndiyo unaanza kufanya ,na limekuwa likikukwamisha wewe
kuanza kufanya jambo unaloliamini,na unasogeza kila siku na siku zina zidi
kwenda mbele
·
WENGI KUTOKUJUA NGUVU NA THAMANI YA
MALENGO YAO
Binadamu tunayo malengo na kila siku huwa mipango na malengo haiishi , na ni kwanini kile ambacho tunacho au
tumekipanga hakitimii, kubwa ni hatujui nini thamani ya nini kile
tunachokiwekea malengo na nguvu yake pale tutakapoamua kukifanya
·
KUJIONA KUWA NI WADOGO
Kutokana na mazingira ambayo yamekuwa yakituzunguka na jinsi
tulivyozoezwa na jamii , wengi hatuanzishi
ndoto zetu kwa kuwa tumekuwa tukijiona kuwa ni wadogo kiumri na kuwa
hatuwezi kufanya mambo makubwa duniani, hivyo kujikuta tunahairisha mambo
mengi.
·
KUJIONA KUWA HUNA ELIMU YA KUTOSHA
Na hii ndiyo tatizo zaidi mtu kujidharau mwenyewe na kujiona kuwa hana
kabisa elimu na hofu kubwa kutokana na elimu ya darasani alipoishia anajiona
hawezi kuanzisha kitu chochote kipya ambacho kitaigusa jamii, na hata ambacho
hakijawahi kuwepo. Kuwaza kuwa wanaostahili ni wenye degree, au diploma au
wanaojua kingereza tuu
·
KUTOKUPATA
MSAADA
Ni hatari Kwa kila mara kujiandaa kupokea msaada Kwa watu wengine, Na
hivyo msaada usipotokea unashindwa kuendelea kufanya kitu chako na kujitegemea
mwenyewe hivyo kujikuta unahairisha kila jambo ambalo unapenda kulifanya katika
maisha. Ikiwa umejisikiliza ndani yako basi usihofu kuanza kwa kisingizio cha
kukosa msaada
·
KUPENDA KUJILAUMU NA KUTAFUTA MTU WA
KUMLAUMU
Wengi wetu na hususani watanzania vijana tunapenda kujilaumu na kutafuta
mtu wa kumlaumu pale mambo yanapokuwa magumu na hivyo kushindwa kuanzisha jambo
jipya katika maisha, na kujikuta kila siku unatafuta mtu wa kumlaumu, kusogeza
jambo
RESPECT TO YOU AND ASANTE KWA KUNIONGEZA UMENIFANYA NIZIDI KUAMINI KWAMBA HAPA NILIPO NI SAHIHI SAANA ASANTE NA UBARIKIWE SANA...
ReplyDeleteNASHUKURU SANA NDUGU YANGU, NAAMINI KWA PAMOJA TUTAYAFIKIA MAFANIKIO YETU, ZIDI KUISOMA BLOG YETU
Delete