.

.

MUNA TOYS & STATIONERY

MUNA TOYS & STATIONERY

Thursday, July 9, 2015

RUNGWE ENEO LINAONGOZWA KWA UKIJANI

Rungwe ni moja ya  wilaya iliyo katika mkoa Mbeya ambayo ni maarufu kwa kilimo cha Migomba, na chai na vilimo mbalimbali katika wilaya hii, kama miwa,mihogo
Na njia ya barabara ya kutoka Mbeya mpaka Rungwe ni njia ambayo inapitika kwa urahisi zaidi na nimiongoni mwa rami bora sana kwa Tanzania
Hali ya hewa ya tukuyu au rungwe ni hali ya ubaridi na inayopendwa na wengi sana kutokana na ukijani uliopo katika eneo zima na njia ya kuelekea rungwe

   Hii ni nyumba ambayo inajengwa na mtoto mwenye umri wa miaka 13 na yeye anaishi humu akiwa amejitenga nje kidogo na wazazi, na huku ni kawaida kwa watoto wakifikia umri huu kujijengea nyumba za kuishi

 Eneo la vijijini kuna usalama na humo ndimo kijana anaishi aliye kidato cha kwanza , anakula kwa wazazi anaishi kwake

   ujenzi huu utumia nyasi, mianzi, tope za ufinyanzi na chini huwa kunasilibwa na udongo mfinyanzi
    Chanzo cha maji ambacho wakazi wa tukuyu(masoko) wamekuwa wakikitumia kwa shughuli za majumbani

                                          kijana akiwa kaanika nguo eneo la getho lake
                                    Ukiambiwa migomba huku ndiyo mahali pake
                           huku kwetu ukiaga unaenda tukuyu bhasi utaagizwa matoki(ndizi) au maziwa

0 comments:

Post a Comment

 

Bongo Blogs - Blog ya Taifa

COPYRIGHT © Egy business solution DESIGN BY NANG JET 0764504595,0672804085