.

.

MUNA TOYS & STATIONERY

MUNA TOYS & STATIONERY

Sunday, March 15, 2015

VIJANA WA JIJI LA MBEYA TULIVYOENDA KUMTEMBELEA MTOTO COSMAS BARAKA ALIYEKATWA MKONO, ILIKUWA HIVI

” SIO WOTE AMBAO TUNAWEZA KUFANYA MAMBO MAKUBWA, BALI TUNAWEZA KUFANYA MAMBO MADOGO SANA KWA UPENDO MKUBWA”

huku tukiongozwa na kauli mbiu inayosema MIMI NITAKULINDA DAIMA vijana mbalimbali wajiji la mbeya na waliopo nje tuliweza kuchangisha kiasi cha Tsh LAKI MOJA NA ELFU TANO MIA TANO(105,500) kwalengo lakifariji familia ya mtoto Cosmas aliyekatwa mkono.

Ziara hii iliandaliwa na taasisi ya MBEYA YOUTH'S pamoja na YWCA MBEYA ambapo ili husisha watu mbalimbali waliopo ndani ya jiji la Mbeya na nje.
dhamira yetu kuu ilikuwa ni kumfariji mtoto na mama yake ambao kwa sasa wanaishi kwa hofu sana sana. Mtoto COSMAS (umri miaka 6) alikatwa na kuondolewa kiganja chake cha mkono na watu wasiojulikana huko maeneo ya RUKWA ,kwa sasa yupo katika hospitali ya RUFAA MBEYA akiendelea na matibabu vizuri.

Familia hii bado ina uhitaji mkubwa sana wa kifedha na ulinzi ili maisha yao yawe salama sana.
MTOTO COSMAS ni zaidi ya unavyomuona katika picha, kiukweli anateseka sanaa, WANAHITAJI MCHANGO WAKO WA HALI NA MALI SANA,

Tunatoa shukrani kwa redio za SWEET FM , na ROCK FM kwa moyo wa kujali na kutuwezesha kusikika maeneo mbalimbali juu ya kilio cha vijana wa jiji la Mbeya na watanzania kwa ujumla kuhusiana na utesaji wa mtoto baraka
UKISUKUMWA KILA MARA NENDA KAMFARIJI MTOTO COSMAS  BARARA
 ELLY BONKE(aliye mbeba mtoto cosmas) Mama wa mtoto, pamoja na ROBERT ELIAH
                             Safari ya kuelekea ndani ya hospital ya rufaa katika WODI no 8, alimolazwa

                                           Tukitafakari juu ya tukio la mtoto kukatwa mkono
           Shadrack na Herman vijana wa jiji la Mbeya miongoni wa waliojitokezaa kumfariji
        EDDY CHONGOLO (mtangazaji wa ROCK FM) akifanya mahojiano na baadhi ya vijana
 JULIUS JAIRO na DEBORA NJULUMI wakikabidhi msaada wa TSH 105,500 kwa mama wa COSMAS
                    Sefania Kajange na Robert Eliah wakiwa na watoto tulioenda kuwaonaa

              Shah Mjanja akiwa pamoja na mtoto COSMAS BARAKA aliyekatwa mkono
                             mama wa mtoto akisimulia namna ilivyokuwa na walivyovamiwa
                                   Mtoto baraka mwenye umri wa miaka 6 aliyekatwa mkono

TUNAWASHUKURU NYOTE MULIOWEZA KUCHANGIA KWA AJILI YA MTOTO COSMAS, TUZIDI KWENDA TENA NA TENA
UKITAKA KUWASILIANA NASI 0764761900

0 comments:

Post a Comment

 

Bongo Blogs - Blog ya Taifa

COPYRIGHT © Egy business solution DESIGN BY NANG JET 0764504595,0672804085