.

.

MUNA TOYS & STATIONERY

MUNA TOYS & STATIONERY

Monday, July 21, 2014

"KWA TAARIFA YAKO WAPINGAJI NI WENGI KULIKO WATAKAO KUTIA MOYO, ANZISHA JAMBO LAKO UNALOLIAMINI"




   
Unaogopa kuanzisha jambo unaloliamini katika ndoto zako, kwa kuhofia watu kukupinga, marafiki au ndugu kwa taarifa yako dunia inawapingaji na wakatishaji tamaa wengi kuliko hata watu ambao wanaweza kukutia moyo. 


Jambo linaloweza kuwa la busara sana kwako ni wewe kutazama ndani yako unaona nini ambacho si rahisi kwa mtu mwingine kujua malengo na nia iliyomo ndani yako. Inakuwa ngumu kwa  mtu aliyeko nje kujua wewe unataka kufika wapi na una malengo yapi?. 

Watakuja hata uliokuwa unawaamini kuwa watakusaidia katika mambo mbalimbali  watakupinga na tena sio kukupinga kwa kikwango kidogo, ni sana na watalenga kukunyamazisha hata uwezo uliokuwa ndani yako usionekane tena.

 lililo jema sana kwako wewe ni kutokusikiliza namna ya wengine wanakatishaje tamaa na wanasimuliaje  namna  usivyoweza kufanikiwa katika jambo unalotaka kulianzisha.

Asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa duniani leo hii walipingwa sana lakini ubishi na uking’ang’anizi wa ndoto na jambo waliloliamini ndiyo uliowafikisha mahali walipo na hatimaye wakafanikiwa sana.

 USIOGOPE, UNAVYOPINGWA NA WALA WAPINGAJI NA WAKATISHAJI TAMAA HAWATAISHA DUNIANI KAMWE, TAZAMA UNAONA NINI NDANI YAKO? NA TENDA KWA BIDII

0 comments:

Post a Comment

 

Bongo Blogs - Blog ya Taifa

COPYRIGHT © Egy business solution DESIGN BY NANG JET 0764504595,0672804085