Maadhimisho ya YOUNG
WOMEN’S CHRISTIAN ASSOCIATION(YWCA) kanda ya kusini
yalivyofana katika wilaya ya Rungwe mwaka huu 26/4/2014 kwa kufanya matukio
mbalimbali, maadhimisho haya yalihusianisha
kanda ya kusini ikiwa ni matawi
yalio katika mikoa ya MBEYA na IRINGA ambapo ilikutanisha tawi la Ywca Mbeya mjini, Ywca mbozi, Ywca rungwe, na tawi la Ywca ilula
Maadimisho haya yaliendana na shughuli mbalimbali za kijamii katika wilaya ya rungwe ambalo ndilo lilikuwa
eneo lililofanyika maadhimisho mwaka huu na shughuli kuu mwaka huu zilikuwa ni
pamoja
1. UFAGIAJI WA STENDI YA TUKUYU NA NJIA YA KUELEKEA OFISI ZA
MKUU WA WILAYA
2. KUTEMBELEA KITUO CHA WATOTO WANAOISHI NA ULEMAVU KATIKA
ENEO LA KATUMBA
3. MAANDAMANO KWA LENGO LA KUTOA UJUMBE KWA JAMII,
ulioendana na upingaji wa ukatili wa kijinsia
4. TUKIO LA PAMOJA NA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE
Maadimisho haya sana
yalilenga kutoa na kupinga ukatili wa kijinsia uliopo miongoni mwa wanajamii ambao tunaishi nao katika jamii
zetu,
mgeni rasmi wa maadimisho haya ya kanda alikuwa ni ndg
CLISPIAN MEELA ambaye ni mkuu wa wilaya
wa rungwe, ambae aligusia mambo mbalimbali yahusuyo jamii yetu na kusisitiza wanawake kutumia fursa za kijamii
MATUKIO YA PICHA JINSI ILIVYOKUWA
wanachama wa YWCA KANDA ya kusini wakiwa katika picha ya pamoja eneo la tukuyu mjini
wakiwa katika ufagizi wa barabara eneo la tukuyu
katibu wa YWCA tukuyu akiwa katika ufagizi wa mji
wanachama wakijiandaa kuingia shule ya watoto wenye ulemavu KATUMBA
mkuu wawilaya akikabidhi bidhaa kwa niaba ya YWCA
MAANDAMANO YA WANACHAMA WA YWCA MJINI TUKUYU
WANACHAMA WAKIWA KWENYE PICHA ZA PAMOJA
MWENYEKITI YWCA KANDA YA KUSINI
PICHA YA PAMOJA NA WATOTO WENYE ULEMAVU




0 comments:
Post a Comment